TFF BADO INAUTAMBUA UONGOZI WA TAREFA

MWENYEKITI WA TAREFA, ALHAJ ISMAIL ADEN RAGE
SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limesema bado linautambua uongozi wa kuchaguliwa wa chama cha soka mkoa wa Tabora (TAREFA), licha ya kuwepo taarifa za kuvuliwa uongozi.
Taarifa iliyotolewa na TFF na kusainiwa na katibu mkuu Angetile Osiah, inasema kuwa kamati yake ya utendaji iliyokutana machi 24 na kuamua kuiagiza kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi ya wachezaji kuuangalia kwa kina mgogoro wa uongozi wa TAREFA na kuutolea uamuzi.
"Kutokana na agizo hilo, TFF itaendelea kuutambua uongozi wa kuchaguliwa wa TAREFA hadi kamati hiyo itakapotoa maamuzi yake.
Viongozi wa TAREFA ni pamoja na ISMAIL ADEN RAGE (mwenyekiti), Albert Sitta (Katibu MKuu) na Yussuf Kitumbo ambaye ni mjumbe wa Mkutano mkuu.

Comments