TAWI LA YANGA UHURU LAMKANA MWANACHAMA ALIYEONGOZA MAANDAMANO YA KUMREJESHA DAVIS MOSHA

KATIBU WA TAWI LA YANGA UHURU BAKARI MPINGO KULIA, AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHISANA NA MWANACHAMA WAO, KUSHOTO NI MMOJA YA MWANACHAMA WA TAWI HILO, SHAMTE MOHAMMED. WANACHAMA wa klabu ya Yanga tawi la Uhuru wamesema hawamtambui mwanachama aliyejitambulisha kwa jina la Bakari Omari mwenye kadi namba 0035 ambaye juzi aliendesha zoezi la baadhi ya wanachama kumrejesha madarakani aliyekuwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Davis Mosha. Katibu Mkuu wa tawi hilo Sultan Bakari Mpingo (007394) alisema jana kwamba Omari si muhusika katika tawi hilo kwani alisimamishwa tangu mwezi januari kutoakana na ubadhirifu wa fedha. Alisema, mwanachama huyo akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya uzinduzi wa tawi aliiba kiasi cha shilingi 150,000 na hivyo kufunguliwa mashitaka katika kituo cha polisi Msimbazi, MS/RB/1975/2011.

Comments