TAMASHA LA KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA WATOTO YATIMA SASA LAPELEKWA MIKOANI

BAADA ya kufanikisha uzinduzi wa albamu ya ‘Bonde la Kukata Maneno’ wiki iliyopita ulioambatana na kuchangia ujenzi wa kituo cha watoto yatima cha huduma ya Injili kwa Watoto (HUIWA), mchungaji Maxmilian Machumu anatarajiwa kuzindua katika mikoa ya Arusha, Mbeya, tanga na Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mchungaji Machumu alisema kuwa lengo la kufanya matamasha hayo ni katika kuendeleza kukusanya kiasi cha shilingi mil.120 ambazo zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa kituo hicho.
Alisema, kupitia tamasha lilolofanyika ukumkbi wa Diamondi Jubilee, aliyekuwa mgeni rasmi, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alichangia Mil.10, huku kiasi cha shilingi mil.68 zikiwa ni hadi zilizotolewa na wadau mbalimbali waliojitokeza kuhudhuaria.
Aliongeza kuwa kwa sasa maandalizi ya ujenzi wa kituo hicho yameshaanza ikiwemo mtaalamu kuanza kutathmini jinsi ujenzi utakavyokuwa hivyo amewashukuru wote waliojitokeza sambamba na kuchangia katika tamasha la Diamond Jubillee na kuomba kuungwa mkono katika matamasha ya mikoani.
Mchungaji Machumu aliongeza kuwa anatarajia kutoa albamu itakayokwenda kwa jina la ‘Nani atakwenda badala yake’ ikiwa na nyimbo nane zinazoelezea na kuhamasisha watu, makanisa na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali kusaidia na kuwajali watoto yatima popote walipo nchini.
“Ili kukomboa kizazi hiki ambacho kipo katika mateso makubwa katika jamii na kusaidia serikali katika majukumu yake ya kuwasaidia wananchim, nadhani kwa kufanya hivyo mungu atawawekea mikono ya baraka na kuwaombea wote waliotoa michango yao”, Alisema.

Comments