STARS V AFRIKA YA KATI ZAINGIZA MILIONI 111


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Machi 29, 2011

MAPATO STARS v CAR .

Mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) zitakazochezwa Gabon- Equatorial Guinea mwakani kati ya Taifa Stars na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) lililofanyika Machi 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 110,552,000. Watazamaji 21,117 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa kiingilio cha sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Asilimia moja ya mapato hayo ambayo ni sh. 1,105,520 yatakabidhiwa kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto.


UWAKALA WA WACHEZAJI

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limepanga mtihani wa uwakala wa wachezaji kufanyika duniani kote Machi 31 mwaka huu. Mtihani huo uwa wa sehemu mbili; maswali kutoka FIFA na kwa shirikisho la mpira wa miguu kwa nchi husika. Hadi sasa hakuna Mtanzania aliyeomba kufanya mtihani huo, hivyo kuwa na sifa ya kuwa wakala wa wachezaji anayetambuliwa na shirikisho hilo.


LIGI YA TAIFA 2010/2011

Ligi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa itachezwa Juni mwaka huu ambapo katika hatua ya awali itakuwa na makundi manne. Makundi hayo yatakuwa katika mikoa ya Pwani, Ruvuma, Kigoma na Singida. Kundi la Pwani litakuwa na mabingwa wa Pwani, Dar es Salaam- 1, Dar es Salaam- 2, Tanga, Lindi na Mtwara. Ruvuma ni Mbeya, Iringa, Rukwa, Morogoro, Dar es Salaam- 3 na Ruvuma. Kigoma ni Tabora, Kagera, Kigoma, Shinyanga, Mara na Mwanza wakati Singida ni Arusha, Manyara, Singida, Kilimanjaro, Dodoma na Shinyanga.


TIMU YA U23

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 inatarajia kuwasili leo saa 8 mchana kwa ndege ya Kenya Airways kutoka Cameroon kupitia Nairobi, Kenya. U23 ilikuwa huko kwa ajili ya mechi za awali za Olimpiki ambapo Machi 27 ilicheza dhidi ya wenyeji na kufungwa mabao 2-1. Baada ya kuwasili wachezaji watapewa mapumziko ya siku moja kabla ya kurejea kambini kujiandaa kwa mechi ya marudiano itakayofanyika Aprili 9 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Boniface Wambura, Ofisa Habari

Comments