SINA MPANGO WA KUTOA ALBAMU KWA SASA -SHETTA



“PAMOJA na kuwa nina singo nyingi zilizotayari lakini sina mpango wa kutoa albamu, labda atokee mtu asaidie kufanikisha hilo”.Hiyo ni kauli ya msanii wa muziki wa kizazi kipya anayejulikana kwa jina la Shetta.
Shetta amefikia hatua hiyo kutokana na hali ngumu ya mchakato mzima wanaokumbana nao wasanii na hasa wanaochipukia toka wanapoingia katika medani hiyo, na hasa ikizingatiwa kuwepo kwa ukiritimba katika hilo.
Kwa mantiki hiyo, msanii huyo anasema ataendelea kutoa singo kadiri zinavyohitajika ili mashabiki waendelee kumfahamu sambamba na kupata nafasi ya kutumbuiza katika maonyesho mbalimbali ya muziki.
Shetta ni mmoja kati ya wasanii wanaofanya vema kwa sasa katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya huku singo yake ya ‘Nimechokwa’ ikikimbiza ipasavyo katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni hapa nchini.

Comments