SIMBA YAENDELEA KULA DAWA A-TOWN, KWENDA CONGO IJUMAA


KIKOSI cha Simba kinaendelea kujifua jijini Arusha kujiandaa na mechi yake ya klabu bingwa ya Afrika dhidi ya Tp Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumapili ijayo huko Lubumbashi.
Habari kutoka Arusha zinasema kikosi kinaendelea vizuri na maandalizi licha ya kukabiliwa na majeruhi kadhaa.
Kikosi hicho kinachonolewa na Mzambia Patrick Phiri kitaondoka nchin Ijumaa kwenda Congo tayari kwa mechi hiyo.

Comments