SIMBA WAANZA KUINOLEA MAKALI TP MAZEMBE

MABINGWA wa Tanzania timu ya soka ya Simba wameanza mazoezi ya ufukweni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi yao ya marudiano ya klabu bingwa ya Afrika dhidi ya Tp Mazembe ya Congo utakaopigwa nchini wiki ijayo.
Simba ambayo imeanza kujinoa katika ufukwe wa Coco chini ya kocha msaidizi Amri Said, pamoja na mechi hiyo ya Tp Mazembe pia itacheza na Kagera Sugar jumatatu ikiwa ni mechi ya Ligi Kuu Bara.
Katika mechi ya awali iliyochezwa jumapili iliyopita huko Lubumbashi, Congo, Simba ilitandikwa mabao 3-1.

Comments