SIMBA KWENDA CONGO KESHO

TIMU ya soka ya Simba inatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Lubumbashi, Congo kwa ajili ya mechi yao ya ligi ya mabingwa barani Africa dhidi ya Tp Mazembe ya huko, itakayopigwa jumapili.
Simba iliyotua jijini Dar es Salaam jana ikitokea mkoani Arusha ilipopiga kambi ya wiki moja kujiandaa na mechi hiyo, imeendelea na mazoezi leo katika uwanja wa Uhuru.

Comments