NIZAR KHALFAN KUIKOSA AFRIKA YA KATI

KIUNGO wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya Vancouver Whitecaps FC ya Canada Nizar Khalfan hatoweza jiunga na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inayojiandaa na mechi yake ya kuwania kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Afrika ya Kati utakaopigwa jumamosi kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Nizar ameshindwqa kujiunga na Stars baada ya uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuchelewa kumuandikia barua ya kumuita huku pia ikimuandikia barua binafsi badala ya klabu yake.

Comments