MUSTAFA HASSANALI AENDA KUTAMBULISHA MPYA NIGERIA


Baada tu ya kuzindua kwa toleo la kiafrika ndani ya Movenpick jijini Dar es salaam, mbunifu wa kipekee wa kiafrika toka Tanzania Mustafa Hassanali amealikwa kushiriki katika maonyesho ya mavazi yanayojulikana kama ‘Arise Magazine Fashion Week’ yanayotarajiwa kufanyika tarehe 10 hadi 13 Machi 2011 ndani ya jiji la Lagos Nigeria .
‘Arise Magazine Fashion Week iliyoandaliwa na Nigeria ’s this Day, inanatarajiwa kukusanya wabunifu mahiri wa Afrika wa ndani na waishio nje ya mipaka ya Afrika watakaoonyesha ubunifu wao, huku wakisindikizwa na wasanii maarufu wa muziki kama vile Dbanj, Keri Hilson, and Estelle.
Akizungumzia akiwa ndani ya jiji la Lagos Nigeria , Mustafa Hassanali alinukuliwa akisema kuwa “nimefarijika na kufurahishwa sana kuwa mmoja wa washiriki wa onyesho hili la ‘Arise Magazine’. Kuwa kwangu wa kwanza kwa mara nyingine tena kualikwa katika onyesho hili la wana wa Afrika kunaonyesha kukubalika kwangu kama mbunifu katika jamii ya mitindo kimataifa” alisema Mustafa Hassanali.
Mustafa Hassanali ataonyesha mavazi yake ya kiafrika yaliozinduliwa Dar es salaam tarehe 4 March katika onyesho la Mamma MIA kwa msaada wa Utepe Mweupe, toleo ambalo lililosanifiwa na uzuri wa Bara la Afrika, mg’ao wa miale ya asubuhi ya jua na machweo yake, ukarimu na ucheshi wa watu wake.
“kama hujapendeza, gauni lako halijameremeta, na halina mkia, hilo si gauni la Mustafa Hassanali, kama toleo langu hili nimetumia uhalisia wa kitanzania, khanga na kupambwa kwa thamani na hariri za hadhi.” alijigamba Mustafa Hassanali.
Arise Magazine Fashion Week’ itafanyika katika hoteli ya Federal Palace Ijumaa ya tarehe 11 Machi saa 9 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Comments