MDOGO WA MR.NICE APANIA KUFUATA NYAYO ZA KAKA YAKE


WIGO wa muziki wa kizazi kipya unazidi kupanuaka kila kukicha na sasa ameibuka nyota mpya katika tasnia hiyo, Eugen Mkenda Kijiko ambaye ametoka na singo inayokwenda kwa jina la 'nyuzi sita akimshirikisha Daz Baba.

Pia hivi sasa yupo katika maandalizi ya kutoa wimbo mwingine wenye mahadhi ya muziki wa kufoka foka wenye jina la ‘Dhehebu la Mama’ ukizungumzia maisha yake aliyolelewa katika muziki, ambayo atawashirikisha Albert Mangwea na Mr Blue.

Comments