MAKAMU MWENYEKITI NA KATIBU MSAIDI TASWA WAENDA KOREA KUSINI KUHUDHURIA MKUTANO WA AIPS


VIONGOZI wawili wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), MAkamu Mwenyekiti Maulid Kitenge na Katibu Msaidizi George John wameondoka jana nchini kwenda Seoul, Korea Kusini kuhudhuria mkutano Mkuu wa wa chama cha kimataifa cha waandishi wa habari za Michezo (AIPS).
Mkutano huo wa 74 utaanza leo Machi 22 hadi Machi 27, mwaka huu huko huko Korea, Kusini.
TASWA inaamini mkutano huo utakuwa na manufaa kwa chama pamoja na waandishi wa habari za michezo kwa ujumla hapa nchini kutokana na mada mbalimbali zitakazojadiliwa.
Pia Taswa inawashukuru wote waliofanikisha safari hiyo ambao ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) waliosaidia tiketi za wahusika kwenda Korea Kusini na kurudi Dar es Salaam.
Tunaamini msaada mkubwa wa NSSF na TFF ni ishara ya ushirikiano mzuri uliojengwa baina ya TASWA na taasisi hizo mbili.

Comments