KISURA WA TANZANIA KUPATIKANA LEO KILIMANJARO KEMPISK


LEO ndiyo kilele cha shindano la Kisura wa Tanzania 2010/11, katika Ukumbi wa Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam ambapo wasichana 10 waliofanikiwa kupita katika mchujo uliofanyika mara tano katika kambi ya warembo hao iliyopo katika Hoteli ya Kiromo View Resort, nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo, Pwani, watachuana kuwania taji hilo.Kwa mujibu wa kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), waandaaji wa shindano hilo, kupitia kwa Mwenyekiti na Mwanzilishi wake, Juliana Urio, mshindi atazawadiwa kitita cha fedha taslimu Sh milioni tano pamoja na kuwa Balozi wa Shirika la Family Health International (FHI) kwa mwaka mmoja, ambapo atakuwa akifanya shughuli mbalimbali chini ya shirika hilo. Zawadi nyingine zitakazotolewa katika shindano hilo ni ofa ya kusomeshwa bure kwa mmoja wa visura hao katika chuo cha mmoja wa wadhamini wa shindano kiitwacho Pure Academy.Pia, FHI watatoa zawadi nyingine tatu za fedha taslimu kwa vikundi vitatu vilivyofanya vizuri katika mpango wa kutoa ujumbe mzuri juu ya elimu ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wananchi, zaidi ikiwa ni janga la ukimwi, kwa wakati wote visura hao walipokuwa kambini. Zawadi hizo ni Sh milioni 1,400,000 kwa kikundi cha kwanza, wakati kikundi cha pili kitapata Sh 1,050,000, huku cha tatu kikijizolea Sh 700,000. Vile vile, BTA itatoa ofa ya kumsomesha mrembo mmoja katika chuo chochote kulingana na mapendeleo yake.Visura watakaochuana leo na mikoa wanayotoka katika mabano, ni Glory Msangi (Arusha), Lilian Busa (Mara), Susan Manoko (Dar es Salaam), Joyce Joseph (Dar es Salaam), Neema Sele (Arusha), Flaviana Makungwa (Dodoma), Grace David (Dar es Salaam), Silipa Swai (Mwanza), Letina Christopher (Dar es Salaam) na Neema Kilango (Arusha).Visura wote waliofanikiwa kuingia katika kambi ya Kisura wa Tanzania mwaka huu, walipata nafasi ya kufundishwa mambo mbalimbali, zaidi ikiwa ni jinsi ya kujitambua wakiwa kama wasichana wadogo wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali katika jamii. Pia, Visura hao wamekuwa wakiandaliwa kukabiliana na changamoto tofauti watakazokabiliana nazo, katika nyanja za kiuchumi, afya, kijamii, siasa na nyinginezo. Pamoja na kuwa shindano hilo linahusu kumtafuta mwanamitindo (model) ambaye atafanya shughuli zake ndani na nje ya nchi, malengo makuu ya shindano la Kisura wa Tanzania ni kuwajengea uwezo watoto wa kike kwenye kiwango cha uelewa na kujitambua katika mabadiliko ya tabia, kwa kuwapa elimu iliyopo katika mfumo rasmi (shuleni) na ile iliyopo nje ya mfumo rasmi.Vile vile, shindano hilo linalenga kuwafundisha visura masuala ya uzazi, afya pamoja na jinsi ya kujikinga na magonjwa hasa ugonjwa wa ukimwi. Kuwafundisha wasichana hao ujasiriamali ili waweze kuwa vinara wa mabadiliko katika maisha yao na kwa taifa zima kwa ujumla na kuwajengea uwezo katika masuala ya uongozi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye. Shindano la Kisura wa Tanzania, linawatumia wanamitindo kama nyenzo ya kuelimisha na kufikisha ujumbe kwa jamii ya kitanzania. Warembo hao mwishoni mwa wiki iliyopita walifanya mahojiano na waandishi wa habari juu ya matarajio yao kueleka shindano lao, wakisema:

Comments