KIJOTI AZIKWA, NCHIMBI KUONGOZA DUA YA KUOMBEA MAREHEMU KESHO

Mwili wa Marehemu Issa Kijoti, Mwimbaji wa Five Star Morden Taarab aliyezaliwa Novemba 21 1985 ukizikwa jana katika maziko yaliyofanyika katika makaburi ya Mtoni Sabasaba jana mara baada ya kuwasili kutoka Mkoani Morogoro ambako marehemu na wengine walipoteza maisha.Chanzo ni http://www.globalpublishers/.

WAZIRI wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi kesho anatarajiwa kuwaongoza wafiwa wa wanamuziki 13 wa kundi la taarab la Five Stars katika dua ya pamoja iliyoandaliwa na Taasisi ya Sanaa Tanzania (SHIWATA) itakayofanyika katika ukumbi wa Star Light jijini Dar es Salaam.

Sambamba na Nchimbi dua hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na Kurugenzi ya Utamaduni sambamba na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Katibu Mkuu wa Shiwata, Suleiman Pembe alisema pamoja na Nchimbi dua hiyo itashirikisha wadau mbalimbali wa sanaa

Pembe alisema dua hiyo itamuhusisha pia aliyekuwa mwanamuziki wa wa bendi ya Wazee Sugu, Mzee Moto aliyefariki dunia juzi katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Aidha Pembe alisema Shiwata wamejipanga kukusanya fedha kupitia michango kutoka kwa wanachama wake ambako wamepanga kila mwanachama kuchangia sh 1000.

“Shiwata imeonelea kuwasaidia wafiwa ambao pamoja na msiba wanakabiliwa na madeni na vitu vingine ambavyo vitaondoa baadhi ya masuala sambamba na waliojeruhiwa kupatiwa matibabu kupitia msaada huo.

Comments