FOMU KUWANIA UONGOZI TAWI LA SIMBA TABORA KUANZA KUTOLEWA KESHO


FOMU za kuwania uongozi wa tawi la Simba jijini Mwanza zinaanza kutolewakesho na zitakuwa zikipatikana katika jengo la CCM Makao Makuu jijini Mwanza.
Akizungumza na Tanzania Daima jana Mwenyekiti wa tawi hilo, Omary Makoye alisema mwisho wa kurudisha fomu hizo ni Aprili 10 ambako alitoa wito kwa wadau wa Simba kujitokeza kuwania uongozi wa tawi hilo.
Makoye alisema uchaguzi Mkuu wa tawi hilo unatarajia kufanyika Aprili 17 wakati nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu, Katibu Mkuu, Msaidizi, Mweka hazina, msaidizi, wajumbe sita wa Kamati ya Utendaji, msemaji na nafasi moja ya ujumbe kwa wanawake.
Makoye alisema sifa mojawapo ya wagombea ni lazima awe mwanachama wa Simba ambaye ana nia thabiti ya kuongoza tawi hilo.

Comments