FLAVIANA MATATA KUZINDUA TAASISI YAKE MEI 21


MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania anayefanya shughuli zake hizo katika nchi za Marekani na Ulaya, Flaviana Matata, Mei 21 mwaka huu, anatarajia kuzinduarasmi taasisi yake ya Flavian Matata Foundation yenye lengo la kusaidia wanawakena watoto kwa ujumla.

Flaviana ambaye aliwahi kuwa Miss Universe Tanzania 2007, anatarajia kuitumiasiku hiyo kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake na watoto, zaidiakilenga katika kupunguza kama si kukomesha mimba za utotoni. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, Flaviana amesema kuwaameamua kuzindua taasisi yake siku hiyo, kwa kuwa ni kumbukumbu ya maelfu yawatu waliopoteza maisha katika ajali ya MV Bukoba iliyotokea mwaka 1996 katikaZiwa Victoria.

Comments