FELLA YUPO BIZE NA ALBAMU YAKE YA TAARAB

SAID FELA
MENEJA wa kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Family, Said Fella, amesema kuwa kwa sasa yuko bize kuimalizia albamu yake mpya, itakayokuwa katika mahadhi ya taarabu.
Fella, alisema amepanga kuiingiza sokoni mapema iwezekanavyo albamu hiyo itakayokuwa na nyimbo sita.
Alisema baada ya kutoa wimbo wa kwanza wa albamu hiyo uitwao ‘Simuachi’ aliomshirikisha Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, sasa anakamilisha nyimbo nyingine.
“Mkubwa kwa sasa nipo bize kumalizia albamu yangu mpya, ambayo nimeamua kuitoa katika mahadhi ya taarabu, hivyo wapenzi wangu wasubiri kupata kazi ya uhakika,” alisema Fella.
Alisema kazi zote za albamu hiyo amepanga kuitengenezea katika studio yao ya Poteza Records iliyopo Temeke jijini, chini ya mtaalamu Sulesh.

Comments