BONDIA KIMONDO KUWANIA UBINGWA WA DUNIA NCHINI URUSI JUMAMOSI


BONDIA Pascal Ndomba ‘Kimondo’, jumamosi hii anatarajiwa kupanda ulingoni nchini Urusi katika pambano la kuwania ubingwa wa Dunia unaotambuliwa na WBC, uzani wa Cruiser.
Kimondo atazipiga na Isa Akberbayev wa Kazakhstan katika pambano la raundi 12 litakalofanyika kwenye ukumbi wa DIVS, Ekaterinburg, nchini Russia.
Kimondo amewaomba Watanzania kumuombea Dua aweze kushinda pambano hilo na kurejea na Mkanda huo wa Dunia, ambao aliso sio utawapandisha chati mabondia wote wa Tanzania.
“Ninaenda kupigania heshima ya Taifa langu, ninawaomba wadau wa ngumi na Watanzania wote waniombee Dua niweze kushinda pambano hilo,” alisema Kimondo.

Comments