ACHENI KUNIJADILI-DAVIS MOSHA


ALIYEKUWA makamu mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga Davis Mosha amewataka baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kuacha kumjadili kwani hana mpango wa kurejea kuiongoza klabu hiyo.
Mosha amesema anashangazwa na baadhi ya wanachama kumfanya ajenda katika vikao wavyoitisha ama kutaka kuitisha kitu ambacho si sahiihi.
Alisema haoni mantiki yoyote kwa wanayanga hao kumjadili kwa sababu uamuzi aliouchukua ni sahihi, hivyo wanatakiwa kujadili ni jinsi gani wataongoza klabu na mambo mengine lakini si yeye.
“Mimi nawaomba waache kunijadili kwani tayari nimejitoa kuiongoza, kufanya hici sikulazimishwa na mtu hivyo sidhani kama ni sahihi kufanya hivyo, wanatakiwa wajadili mambo yenye manufaa kwa klabu si Mosha kujiuzulu kwake”, Alisema.

Comments