ZAHANATI YAUA MZAZI, KISA KUKOSA 100,000


Upendo Simon na Chalila Kibuda

DISPENSARI ya Community Oral Health (COH)ya Gongola mboto Mazizini jijini Dar es Salaam inaendesha huduma ya kuzalisha wakati haina hadhi hiyo na kusababisha kifo kwa mwanamke aliyekwenda kujifungua .
Tanzania Daima ilifika katika Dispensari hiyo na kujiona hali ambavyo inaendesha huduma ya uzazi wa kwa wanawake wanajifungi ambapo ilibainika haina uwezo huo na kusababisha kifo cha Mwanamke Issabella Mganga ambaye alifariki kutokana na kuishiwa damu baada ya kujifungua .
Kifo cha Issabella Mganga alijifugua watoto mapacha na kuishiwa damu hali ambayo Dispensari hiyo haikuwa na huduma ya kuongeza damu kwa mwanamke huyo.
Tanzania Daima iligundua kifo cha marehemu Mganga kilitokana na kuishiwa damu baada ya kujifungua ili gundulika kuwa dispensary hiyo inajali fedha kuliko utoaji wa huduma .
Akizungumza Tanzania Daima Dispensari hiyo Ndugu wa Maremu Jairosi Mganga alisema kifo hicho kilitokana na huduma finyu inayotolewa na dispensary hiyo .
Alisema kuwa kutokana na masuala ya uzazi ambayo yanahitaji damu kulikuwa hakuna haja ya kupokea kama kulinda uhai wa mtoto na Mama.
Hata hivyo Mganga alisema kuwa Muuguzi aliyekuwa zamu siku hiyo alizidi kumchoma sindano tu bila ya kumuongezea damu mgonjwa huyo na alipoulizwa kwa nini hakumuongezea da alisema pale wao hawana benki ya damu.
“Tunatoa huduma nyingi tu ikiwemo ya kuzalisha wakinamama lakini kuhusu kumuongezea mtu damu hatujihusishi na hutoaji wa huduma hiyo”alisema muuguzi
Sababu kubwa ya marehemu huyo kufariki Dunia ni kukosekana kwa fedha 158,000 katika dispensary hiyo ndiyo maana hawakumpa ushirikiano wa kutosha mama aliyejifungua mapacha.
Baada ya kutokea tukio hilo Mmiliki wa Dispendari hiyo alitoweka katika mazingira ya kutatanisha na juhudi za Tanzania Daima ziliishia hapo .

Comments