YANGA YAHOFU KUHUJUMIWA SONGEA

LLOYD NCHUNGA, MWENYEKITI WA YANGA

SAA chache kabla ya kushuka dimbani kukwaana na Majimaji mjini Songea, vinara wa ligi kuu bara Yanga imedai kuwepo na dalili za kufanyiwa kwa hujuma katika mechi yao hiyo.

Akizungumza kwa simu kutoka Songea, mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga amesema kuwa wamebaini hali hiyo kupitia makachero wao na wameapa kujidhatiti kwa hali yoyote itakayotokea.....
"tumepata taarifa kuwa wamepanga kutuhujumu katika mechi yetu, ila tutakuwa makini kwa lolote litakalotokea",Alisema Nchunga.

Comments