WASANII KIBAO KUPAMBA UZINDUZI WA TOP C CLUB BILICANAS SIKU YA VALENTINE


WASANII mahiri wakiwemo Diamond, Mr.Chocolate, Q-Chillah, Sam wa Ukweli na H-Baba wanatarajiwa kupamba uzinduzi wa albamu ya msanii wa bongo fleva anayekwenda kwa jina la TOP C inayokwenda kwa jina la LOFA siku ya Februari 14 'Valentines Day' katika ukumbi wa CLUB BILICANAS.

Meneja wa msanii huyo Babuu Kisauji amesema kwamba maandalizi yanakwenda vizuri na kwamba kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa mashabiki watakaojitokeza katika uzinduzi huo zikiwemo tisheti zenye nembo ya msanii huyo ambapo kiingilio kitakuwa sh.10,000 kwa kila mtu.

Comments