WANACHAMA YANGA WASISITIZA UKAGUZI WA MAHESABU, WASEMA WASIOMTAKA MANJI WAONDOKE WAO




BAADHI ya wanachama wa klabu ya Yanga wameunga mkono zoezi la ukaguzi wa hesabu za klabu hiyo ambalo lilipendekezwa na mfadhili na mjumbe wa bodi ya udhamini wa klabu hiyo, Yusuf Manji.
Pamoja na kuunga mkono huko, wanachama hao wamewataka wanachama wasiotaka uwepo wa Manji katuika klabu hiyo kuondoka wao kutokana ukweli kwamba kuna baadhi ya viongozi ambao wameondolewa ndani ya uongozi walikuwa wananufaika kwa migongo ya Yanga.
Wakienda mbali zaidi, wanachama hao ambao waliongozwa na matawi 26 ya mkoa wa Dar es Salaam walinmtaka mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd Nchunga kuitisha mkutano wa wanachama ili kuwajadili wanachama wakorofi

Comments