WANACHAMA YANGA WACHARUKA

BAADHI ya wanachama wa klabu ya soka ya Yanga wamemjia juu mfadhili wao Yusuf Manji na kudai kuwa ndiye chanzo cha migogoro ya hapa na pale inayoendelea hivi sasa katika klabu hiyo.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) wanachama hao toka tawi la Tandale Uzuri walisema kwamba Manji amekuwa akitumia baadhi ya wenzao katika kufanya mambo yenye manufaa kwake.
Walidai kuwa baadhi ya mambo amekuwa akiyafanya kwa njia za panya hivyo kama anataka kuendelea kuwepo Yanga ni lazima aweke wazi mambo anayoyafanya.
"Hali hii imetuchosha kwa kweli kama Manji anataka kuwa nasi nibora awe muwazi katika mambo anayoyafanya, si kutumia baadhi ya yao katika kujinufaisha", Alisema mmoja ya wanachama.

Comments