VODACOM TANZANIA YATANGAZA ZAWADI ZA 5KM FUN RUN.


RUKIA MTINGWA, MENEJA UDHAMINI WA VODACOM

Moshi, Februari 25 2010.
Vodacom Tanzania imetangaza rasmi zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa riadha za Vodacom 5km fun run ambazo zitafanyika Tarehe 27 pamoja na mbio kubwa za 42km Kilimanjaro Marathoni 2011 mkoani Kilimanjaro. Udhamini huo ni wa mbio fupi za burudani maarufu kama Vodacom 5KM FUN RUN.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi, Meneja Udhamini wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa, alisema kwamba katika mashindano hayo Vodacom imejiandaa na kujipanga vyema ili kuhakikisha mbio hizi za burudani zinakuwa na msisimuko na mvuto kwa wakimbiaji wengi hususani wale wapenzi wa mbio fupi.
Kama ilivyokuwa ada ya mbio hizi washiriki wote watakaomaliza mbio hizi watakuwa ni washindi na Vodacom itawazawadia zawadi kem kem.
Alisema mashindano ya mwaka huu yatakuwa na hamasa kubwa kwani uzoefu unaonyesha kwamba kila mwaka idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka na anatoa wito kwa watu wanaotaka kushiriki mbio hizo wazidi kujitokeza na kujiandikisha pale Keys Hotel iliyopo manispaa ya moshi.
Mtingwa alisema ili kuleta washindi wote watawekewa fedha zao kwa njia ya M pesa palepale uwanjani.Ili kuimarisha kauli mbiu yetu ya PAMOJA DAIMA.
Akizitaja zawadi hizo alisema mshindi wa kwanza atajinyakulia shilingi 100, 000,wapili shilingi 80,000,watatu shilingi 60,000,wanne shilingi 50,000,watano 40,000,na kuanzia mshindi wa tano mpaka wa tisa watapatiwa kifuta jasho cha shilingi 20,000 kila mmoja na kuwekewa muda wa maongezi kwenye simu zao wenye thamani ya shilingi 20,000,Alisema Mtingwa”
“Pamoja na udhamini huu Vodacom inaamini kuwa itakuwa inaunga mkono juhudi za serikali za kunyanyua na kukuza vipaji vya wanamichezo hapa nchini ambao hapo baadaye wataweza kulitangaza Taifa letu katika nyanja za michezo za kimataifa.
Zaidi ya hayo tunashiriki mashindano haya ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali yetu za kukuza sekta ya utalii, hasa ukizingatia mashindano haya yanafanyika mkoani Kilimanjaro chini ya mojawapo ya vivutio vikuu vya utalii kama vile Mlima mrefu barani Afrika, Mlima Kilimnjaro.
“Vodacom Tanzania itaendelea kudhamini michezo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kukuza viwango vya michezo hapa nchini na hatimaye kuliletea taifa letu heshima katika mashindano ya kimataifa’.
Baadhi ya michezo inayodhaminiwa na na Vodacom ni pamoja na Mpira wa Miguu,Vodacom Miss Tanzania, mashindano ya kuogelea mbio za boti na mbuzi.

Comments