VIINGILIO SIMBA VS ELAN de MITSOUDJE HIVI HAPA

MAKAMU MWENYEKITI WA KLABU YA SIMBA GEOFREY NYANGE 'KABURU' AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA MECHI YAO YA LIGI YA MABINGWA BARANI AFRIKA DHIDI YA ELAN de MITSOUDJE YA COMORO JUMAPILI, KULIA NI MSEMAJI WA TIMU HIYO, CLIFFORD NDIMBO.

WAKATI Simba ikijinasibu kuibuka na ushindi katika mechi yao ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Elan de Mitsoudje ya Comoro jumapili hi kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, kingilio cha juu katika mechi hiyo ni sh.20,000 kwa watakaokaa katika viti maalum (VIP), imefahamika.

Ofisa habari wa Simba Clifford Ndimbo amesema kwamba watakaokaa jukwaa kuu watalipa sh.15,000, huku watakaokaa jukwaa la kijani watalipa sh.8,000 na wale watakaokaa mzunguko watalipa sh.3,000.

Kabla ya mechi hiyo kutatanguliwa na mechi ya kirafiki baina ya timu ya Vijana ya Simba dhidi ya Downbrokers.

Comments