VIFAA VIPYA VYA TWANGA PEPETA VITAONEKANA LEO BILICANAS

ASHA BARAKA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA BAADHI YA WASANII WAPYA WA TWANGA PEPETA AMBAO WATAONEKANA KWENYE ONYESHO LA LEO KATIKA UKUMBI WA CLUB BILICANAS.


HADIJA MNOGA AKA KIMOBITEL, HUYU AMERUDI NYUMBANI.


NADHANI kila mdau wa burudani anafahamu kwamba wiki iliyopita bendi ya EXTRA BONGO ilichota wasanii 8 toka African Stars 'Twanga Pepeta', lakini hiyo sio issue Wadau kwani Twanga Pepeta ni kitivo cha mafunzo bado inaendelea kusongesha.

Asha Baraka, Mkurugenzi wa bendi hiyo amesema kwamba hakuna lililoharribika kwani kuna vichwa vimeshaziba hivyo mambo yanakwenda kama kawaida.

Ukitaka kuhakikisha maneno ya Asha jongea mjengoni (bilicanas)usiku wa leo ujionee, kama ukishindwa ibukia katika maonyesho yake mengine.

Comments