TFF CHAKACHUA RATIBA LIGI KUU YA VODACOM


SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limebadilisha ratiba za baadhi ya michezo ya ligi Kuu Tanzania bara hatua ya lala salama iliyoanza Januari 15 katika viwanja mbalimbali hapa nchini.

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema mabadiliko hayo yanaihusu michezo namba 85 kati ya Azam FC na Toto Africans iliyokuwa ichezwe Februari 2 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam imesogezwa mbele hadi Februari 4 kwa sababu katika uwanja huo kutakuwa na mchezo kati ya Yanga na Mtibwa Sugar.

Mchezo mwingine ni namba 89 kati ya Polisi Dodoma na Simba uliokuwa uchezwe Februari 5 umesogezwa mbele kwa siku moja kutokana na uwanja huo ulio chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM), siku hiyo kutakuwa na sherehe za miaka 34 ya CCM.

Mchezo namba 90 kati ya JKT Ruvu na African Lyon uliokuwa uchezwe Februari katika uwanja wa Uhuru umesogezwa mbele hadi Februari 7.

Aidha Wambura alisema mchezo namba 96 mchezo mwingine uliosogezwa mbele kati ya Kagera Sugar na Yanga uliokuwa uchezwe Februari 16 hadi 17 kutokana na mchezo wake wa marudiano wa Kimataifa kati yake na Dedebit ya Ethiopia unaotarajia kuchezwa Februari 11 na 13.

Comments