TENGA AKIPONGEZWA BAADA YA KUSINDA UJUMBE CAF


Rais wa TFF, Leodegar Tenga akipongezwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Uganda (FUFA) Lawrence Mulindwa mara baada ya kuchaguliwa Februari 23 mwaka huu kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Afrika (CAF) katika uchaguzi uliofanyika jijini Khartoum, Sudan.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani (kushoto) na Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye wakimpongeza Rais wa TFF, Leodegar Tenga baada ya kuchaguliwa Februari 23 mwaka huu jijini Khartoum, Sudan kuingia kwenye Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika Tanzania (TFF), Leodegar Tenga akiwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kumchagua Februari 23 mwaka huu kuingia kwenye Kamati ya Utendaji jijini Khartoum, Sudan.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) wakimpongeza Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Leodegar Tenga baada ya kuchaguliwa Februari 23 mwaka huu jijini Khartoum, Sudan kuingia kwenye Kamati ya Utendaji.

Comments