SIMBA YAKAMATA USUKANI LIGI KUU BARA!!!!


MABINGWA wa ligi kuu bara timu ya soka ya Simba imefanikiwa kuongoza ligi hiyo baada ya kuishinda Polisi Dodoma kwa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Jamhuri mjini Dodoma.

Mabao ya Simba yalifungwa na mshambuliaji wake mahiri Musa Mgosi katika dakika ya 54 na 84, hivyo kuifanya kufikisha pointi 33, ikifuatiwa na mahasimu wao Yanga yenye pointi 32.

Comments

Post a Comment