SIMBA, ELAN de MITSOUDJE WATAMBIANA

KIKOSI CHA SIMBA
WAWAKILISHI wa Tanzania katika ligi ya mabingwa barani Afrika timu ya soka ya Simba imesema pamoja na ugumu utakaokuwepo katika mechi yao ya kesho dhidi ya Elan de Mitsoudje ya Comoro, wana uhakika wa kuibuka na ushindi.

Kocha mkuu wa Simba Patrick Phiri amesema kwamba amekiandaa kikosi chake ipasavyo na hasa baada ya kuwasoma wapinzani wao katika mechi ya awali waliyocheza ugenini wiki iliyopita.

Naye kocha msaidizi wa Dedebit Yossouf Ahamada amesema kwamba wamekuja kushinda na si kutembea hivyo Simba isubiri kipigo kitakatifu.

Simba inahitaji kuishinda ili kusionga mbele katika michuano hiyo ambapo ikishinda itakutana na mabingwa watetezi Enyimba ya Nigeria.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI SIMBA SPORTS CLUB.

Comments