NURUDIN BAKARI KUWAKOSA WAPALESTINA, WAHABESH


MAUMIVU ya mguu yanayomuandama Nurdin Bakari yamemfanya ashindwe kujiunga na wachezaji wenzake wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' ambayo kesho itashuka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Palestina.

Pamoja na kuikosa mechi hiyom, Nurdin pia atakosa mechi ya marudiano ya kombe la shirikisho baina ya timu yake ya Yanga na Dededebid ya Ethiopia itakayopigwa ugenini mwishoni mwa wiki hii.
Msemaji wa Yanga Louis Sendeu amesema leo kwamba, pamoja na Nurdin majeruhi mwingine katika timu hiyo ni Shephano Mwasyka ambaye anamaumivu ya goti huku kipa Yaw Berko na Ernest Boakye waliokuwa majeruhi wakianza mazoezi baada ya kupata nafuu.
Alisema kikosi cha Yanga kitaondoka alhamis kwenda Ethiopia.

Comments