MIMI NI YANGA DAMU-SABODO

SABODO
MFANTABIASHARA maarufu na kada wa Chama cha MAopinduzi (CCM), Mustafa Sabodo amesema yeye ni mnazi mkubwa wa timu ya soka ya Yanga hapa nchini.

Hata hivyo, Sabodo amesema yupo tayari kuisaidia kwa lolote timu hiyo pamoja na mahasimu wao Simba ili mradi tu viongozi wafike kwake na kuzungumza nae.
"Mimi naipenda sana Yanga...lakini nipo tayari kusdaidia hata Simba pia...kama viongozi wao watakuja na kueleza matatizo ya vilabu vyao nitaangalia nitasaidia kwa kiasi gani", Alisema.
Sabodo amekuwa akisaidia jamii mbalimbali bila kujali itikadi wala imani ya mtu.

Comments