MASHUJAA MUSICA YAIBOMOA DIAMOND MUSICA 'VIJANA CLASSIC'


KUTOKA KUSHOTO NI MARYAM, KELVIN NA SALMA AKA TEKE TEKE

RAPA MPYA SAUTI YA RADI

MENEJA WA MASHUJAA MUSICA MUJIBU HAMIS KATIKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA UTAMBULISHO WA WASANII WAPYA WA TIMU HIYO WALIOWANYAKUA KUTOKA DIAMOND MUZIKA KUSHOTO NI RAPA MIRINDA NYEUSI NA KULIA NI SAUTI YA RADI

KATIKA kujiimarisha kwenye tasnia ya burudani nchini bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa Musica imewanyakuwa wasanii sita kutoka bendi ya Diamond Musica ‘Vijana Classic’ akiwemo Rapa machachari, Sauti ya Radi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwatambulisha wasanii hao wapya kwa wasanii wa habari, meneja wa bendi hiyo Mujibu Hamisi Taratibu alisema hatua hiyo inatokana na ushindani uliopo hivi sasa.
Alisema kwa kuwachukua wasanii hao anaamini bendi hiyo itaweza kwenda sambamba na hali hiyo sambamba na kuziangusha chini bendi zilizokuwa juu.
“Mwaka huu ni wa mapinduzi katikia medani ya muziki wa dansi nchini, tunataka kuziangusha zile bendi ziliozojuu na sisi tulio chini tunataka tupande”, Alisema.
Pamoja na Sauti ya Radi, wasanii wengine walionyakuliwa ni pamoja na Salma Shaban ‘Teke Teke’, Kelvin Katiliga ‘Dume la Ruba’, Maryam Delape, Magreth na Corando ambao wote ni wanenguaji.

Comments