MAKOCHA WANNE WAWANIA KUINOA YANGA


MAKOCHA wanne kutoka nchi tofauti wamejitokeza kuomba kibarua cha kuinoa timu ya soka ya Yanga kurithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mserbia Kostadin Papic.
Papic alijiuzulu kuinoa timu hiyo wiki iliyopita akipinga uongozi kumuajiri kocha mzawa Fred Felix Minziro kama msaidizi wake.

Mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga amesema kwamba kamati ya utendaji itakutana jumatatu ijayo kwa ajili ya kuwajadili makocha hao.

Amesema tayari wameshafanya mazungumzo na mmoja kati ya hao, Sam Timbe ambayo yanakwenda vizuri lakini hatima yake itajukana katika kikao hicho.

Nchunga aliwataja makocha wengine ambao wametuma wasifu wao (cv) kuwa ni Roy Barego wa Uingereza anayeishi nchini Afrika Kusini ambaye aliwahi kuinoa timu ya Taifa ya Zimbambwe, pia mwingine anatoka Yugoslavia na mwingine Serbia.

Comments