LINEX KUUZA ALBAMU YAKE KWA BEI YA JUMLA



MKALI wa bongo fleva Linex amepanga kuuza kwa jumla albamu yake ya pili, lengo ikiwa ni kuondokana na usumbufu toka kwa wasambazaji wa muziki sambamba na unyonywaji wa kazi zao.
"Nitafanya mazungumzo na wasambazaji ili kuweza kumuuzia 'master' ya albamu yangu, atakayekubaliana nami atanipa changu na kumkabidhi...baada ya hapo atajijua kama itakula kwake au akipata faida zaidi yangu mie nshakunja changu", Amesema Linex.
Linex ambaye singo yake ya 'Moyo wa Subira' inashika kasi katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni amesema tayari ameshaanza maandalizi ya albamu yake hiyo.

Comments