KALUNDE BAND KUSHEREHEKEA MIAKA 5 SIKU YA VALENTINE


BENDI ya muziki wa dansi ya Kalunde inatarajia Februari 14 mwaka huu ambayo itakuwa Siku ya Wapandanao 'Valentine Day' inatarajia kusherehekea miaka mitano tangu kuanzishwa kwake.
Mmoja wa viongozi wa bendi hiyo, Junior Gringo alisema burudani hiyo ambayo itaporomoshwa katika Ukumbi wa Reinbow Mbezi itakuwa maalumu kwao pamoja na mashabiki wa bendi hiyo.
Siku hiyo kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa mashabiki watakaofika, ambapo wasanii wa filamu nchini Ray Kigonsi 'Ray' na Steven Kanumba 'Kanumba watatoa zawadi kwa mashabiki hao.
"Tumeamua kuungana na wasanii hawa wa filamu ili kuonesha kwamba tunashirkina kwa pamoja tukiwa kama wote ni wasanii, hivyo kuonesha mshikamono wetu.Alisema licha ya zawadi hizo, bendi hiyo pia itatambulisha nyimbo zake nne ambazo zimekamilika hivi karibuni.

Alizitaja nyimbo zitakazotambulishwa siku hiyo kuwa ni Nyemo ambayo imeimbwa kwa kabila la Kigogo na kutungwa na Sarafina Mshindo.

Nyimbo nyingine ni Gloria iliyotungwa na Shehe Mwakichui, Ndoto ambayo ameitunga yeye mwenyewe na Masumbuko utunzi wake Deo Mwanambilimbi.

Kiongozi huyo alisema kabla ya kufika ya kufika siku hiyo ya Valentine, bendi Februari 12, mwaka huu itawatambulisha wanamuzi wapya katika Ukumbi wa Rainbow.

Aliwataja wanamuziki watakaotambulishwa kuwa ni Remmy Gius ambaye ni mwambaji na mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Edson anayekung'ukuta gita la solo.

Comments