HUU NDIO USHAHIDI WA YUSUF MEHBOOB MANJI

FUSO LIKISHUSHA MAGAZETI YALIYOPELEKWA MAHAKAMANI KAMA USHAHIDI
LUNDO LA MAGAZETI YALIYOPELEKWA KAMA USHAHIDI MAHAKAMANI HAPO

MANJI AKIZUNGUMZA NA WAKILI WAKE MABERE MARANDO

MANJI AKIPATA FEGI HUHU AKIPITIA MAKABRASHA

MANJI AKIWA KORTINI NA WASAIDIZI WAKE
Na Happiness Katabazi
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yusuf Manji(35) jana ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa kashfa zilizotolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd,Reginald Mengi kuwa yeye ni Fisadi Papa zimemvunjia heshima na kusababisha asiaminiwe tena wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Manji ambaye jana ilikuwa ni mara yake ya kwanza kupanda kizimbani hapo , alitoa maelezo hayo wakati akiongozwa kutoa ushahidi wake na mawakili maarufu wa kujitegemea nchini, Mabere Marando, Dk.Ringo Tenga, Richard Rweyongeza, Sam Mapande na Beatus Malima mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana.

Wakati kesi hiyo ya kashfa ya madai ya Shilingi moja iliyofunguliwa na Manji dhidi ya Mengi na Televisheni ya ITV ilipoanza kusikilizwa rasmi mahakamani hapo jana ambapo Manji ndiyo shahidi wa kwanza wa upande wa mlalamikaji kutoa ushahidi wake na msafara wa Manji uliambatana na magari mbalimbali likiwemo gari aina ya Fuso lilokuwa limebeba lundo la magazeti ambayo yalichapisha habari iliyomnukuu mdaiwa akimkashfu mdaiwa ili yatumike mahakamani hapo kama vielelezo.

Manji alieleza mahakama kuwa kupitia Kipindi Maalum kilichorushwa na ITV, April 23-27 mwaka 2009 ambacho kilimuonyesha Mengi akimtaja yeye na wafanyabiashara wengine wanne kuwa ni mafisadi papa, wanaamisha rasilimali za taifa kupeleka nje ya nchi na kwamba wameshiriki kikamilifu katika ufisadi wa ununuzi wa magari ya JWTZ, Rada,Mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma,mifuko ya hifadhi ya jamii ya PSPF na NSSF, Dowans na Richmond ,kutoa rushwa kwa maofisa wa serikali ili waweze kupata tenda za serikali na kwamba fedha walizonazo zimetokana na ufisadia kwaajili ya ufisadi na kipindi hicho cha jana kilionyeshwa kama ushahidi mahakamani hapo na mahakama kupokea DVD ya kipindi hicho kama kielelezo cha tisa.

“Mheshimiwa hakimu kupitia matamshi hayo ya mdaiwa (Mengi) kwenye Kipindi hicho maalum…kwakweli kimenifunjia heshima ndani ya familia yangu, kwa zaidi ya wafabnyakazi 4,000 niliyowaajili kwenye makampuni yangu, kwa wafanyabiashara wenzangu wa ndani na nje ya nchi, jamii inaniona mimi ni mtu mchafu sana na wabunge wamepoteza imani na mimi kwaajili ya matamshi hayo;

“Na kuthibitisha kuwa wabunge hawana imani na mimi hasa wabunge waliokuwa wabunge wa bunge lilopita….kama uchumi ya bunge iliniarika kwenye mmoja ya kikao chao nikatoe hotuba lakini cha ajabu nilivyofika kwenye kikao hicho kuna baadhi ya wabunge wa kamati hiyo walinikataza nisitoe hotuba yangu kwasababu ni mtu mchafu kwenye jamii na Mengi alikwishanitaja adharani kuwa mimi ni fisadi papa na mimi ikaniradhimu niondoke kwenye mkutano huo na kurejea nyumbani.

“Na ninaomba kashfa hizo zilizoelekezwa na mdaiwa kwangu mimi si za kweli kabisa kwani misijawahi kujihusisha na biashara za Rada,Dowans, Richmond, ununuzi wa magari ya jeshi, kuamisha fedha hapa nchini kuzipeleka nje ya nchi na wala sijawahi,kushtakiwa kwa kutoa rushwa ili nipate tenda za serikali na hadi nina umri huu sijawahi kutoa fedha zangu mfukoni kujenga nyumba hata moja hapa nchini wala nje ya nchi…hapa jijini naishi kwenye nyumba ya familia pale Upanga na Marekani kuna nyumba ya familia aliyoiacha marehemu baba yangu Meibou Manji.”alidai Manji.

Wakili Marando alipomhoji Manji anatafsri vipi neno fisadi papa aliloitwa na Mengi; Manji alijibu kuwa analitafsiri kwamba yeye ni mtu anayekabiliwa na maskendo na kwamba Papa ni aina ya samaki mkubwa aishie baharini na kukana kwamba yeye siyo samaki aina ya papa yeye ni binadamu nakuongezwa kuwa hiyo nayo ilichangia kusababisha afikie uamuzi wa kumfungulie kesi hiyo Mengi kwani amemdhalilisha na kumshushia heshima yake vya kutosha waki yeye ni mtu safi na anayeheshimika katika ndani na nje ya nchi.

Manji ambaye aliwasili mahakamani saa 6;07 baadhi ya mawakili na wananchi waliokuwa wamefika mahakamani hapo kwaajili ya kufuatilia kesi zao na za jamaa zao kulazimika kuingia kuingia kwenye ukumbi namba mbili wa mahakama hiyo kwaajili ya kuwahi nafasi ya viti ili waweze kusikiliza kesi hiyo ambayo imeonekana kuvuta hisia za watu wengi na mjadala, wakati akitoa ushahidi wake alitoa nyaraka nane halisi ambazo ni mialiko ya shughuli za kiserikali,ya ndani na nje ya nchi iliyokuwa ikimtaka awe mgeni rasmi katika shughuli hizo na kutoa hotuba mbalimbali za masuala ya kiuchumi,magazeti ya This Day na Kulikoni pamoja na DVD vyote hivyo vilipokelewa na mahakama na kufanya jumla ya vielelezo vilivyopokelewa kuwa tisa.

Nakwamba aliudhulia shughuli hizo na watu walimpokea vizuri na kumpa heshima zote na kwamba kwa kashfa hiyo ya Mengi dhidi yake imefanya wahitimu wa shule mbalimbali alizokwenda kwenye mahafali yao waliyomwalika kama mgeni rasmi hivi sasa wanamtazama kama ni mtu mchafu na mtoa rushwa hali aliyosisiza kuwa imemvunjia heshima na kumpatia wakati mgumu wa katika majukumu yake ya kila siku.

Hakimu Katemana aliairisha usikilizaji wa kesi hiyo hadi leo asubuhi ambayo shahidi huyo Manji atakapoendelea kutoa ushahidi wake na kuhojiwa na mawakili wa Mengi.

Mapema mwaka juzi, Yusuf Manji alimfungulia kesi ya madai ya kashfa Mengi na kituo cha televisheni cha ITV akitaka amlipe fidia ya shilingi moja kwa madai kuwa Mengi alitumia televisheni yake kumkashifu kwa kumuita ‘Fisadi Papa’ na kwamba mmoja wa watu wanaopora rasilimali za Tanzania.mwisho

Comments

  1. Dina hii ni kweli au umekosea mimi naona kama haiwezekani gharama zunazo mgarim Manji halafu adai fidia ya shilingi moja.

    ReplyDelete
  2. Wala cjakosea james ni kweli anataka kulipwa SHILINGI MOJA na kuombwa radhi katika vituo vya mdaiwa wake kwa siku &

    ReplyDelete

Post a Comment