CHUJI, MBUNA WAACHWA SAFARI YA ETHIOPIA

LOUIS SENDEU, MSEMAJI WA YANGA
WAWAKILISHI wa Tanzania katika kombe la Shirikisho timu ya soka ya Yanga inatarajiwa kuondoka kesho kwenda Ethiopia, huku ikiwaacha wachezaji wake mahiri Athuman Idd ‘Chuji’ , Stephano Mwasyika, Nurdin Bakari na Fred Mbuna.

Msemaji wa Yanga Lous Sendeu amesema leo kwamba Mwasyika na Nurdin ni majeruhi huku Mbuna pamoja na wachezaji wengine wameachwa kutokana na mapendekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo, Sam Timbe.

Sendeu alisema msafara wa watu 26 wakiwemo wachezaji 18 na viongozi nane utaondoka kwa ndege ya Shirika la Ethiopia tayari kwa mechi yake dhidi ya Dedebit ya huko itakayopigwa jumamosi katika uwanja wa Adis.


Aliwataja wachezaji watakaondoka kuwa ni pamoja na Yaw Berko, Ivan Knezevic, Shadrack Nsajigwa, Abuu Ubwa, Isaac Boakye, Chacha Marwa, Job Ibrahim, Godfrey Bonny na Davis Mwape, Iddi Mbaga, Juma Seif, Yahaya Tumbo, Omega Seme, Kiggi Makassy, Nsa Job, Nadir Haroub ‘Canavaro’ na Ernest Boakye.

Kwa upande wa viongozi ni pamoja na Mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga, Timbe, kocha msaidizi Fred Felix Minziro, Meneja Salvatory Edward, Daktari Juma Sufiani, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Charles Mugondo, Sendeu na Makamu wa Pili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Athuman Nyamlani ambaye atakuwa mkuu wa msafara.

Comments