AZAM FC YASHIKA USUKANI WA LIGI KUU YA VODACOM



TIMU ya soka ya Azam jana ilitinga kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kuiadhibu JKT Ruvu kwa mabao 2-0 na kuziporomosha Simna na Yanga zilizokuwa zikiwania nafasi hiyo, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kwa msimamo huo Azam imefikisha pointi 35 ikiwa sawa na Yanga lakini inashikilia nafasi hiyo ikiwa na mabao 24, Yanga wana mabao 18 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu ina pointi 34.

Comments