ALI CHOKI HAWEZI KUNIUA, LABDA ANICHOME KISU -ASHA BARAKA

ASHA BARAKA KATIKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI HAWAPO PICHANI, KUSHOTO NI AMIGOLAS NA KULIA LUIZER MBUTU




ASHA AKIWA NA BAADHI YA WASANII WAKE.
MKURUGENZI wa African Stars Entertainment (ASET) Asha BAraka amesema kwamba itakuwa ngumu kwa msanii na kiongozi wa bendi ya Extra Bongo Ali Choki kumuua kwa njia yoyote labda amchome kisu.

Asha ameyasema hayo kwa uchungu kufuatia vita ya chinichini inayoendeshwa nma Choki ili kuhakikisha anammaliza sambamba na kuiua bendi yake ya Twanga Pepeta.

Hatua hiyo inafuatia Choki kunyakua wanamuziki nane wa Twanga wiki iliyopita hali ambayo Asha amesema haiwezi kuua bendi yake wala haiwezi kumfilisi katika mambo yake.

Baraka amesema kwamba Twanga Pepeta ni kama chuo na wasanii wake wote ni nyota hivyo pamoja na Choki kuchota baadhi ya wasanii bado bendi hiyo itaendelea kusimama kama ilivyo.
Akienda mbali zaidi, Asha alisema ameshafahamu njama zote zxa Choki lakini yupo tayari kwa lolote kwan i maisha yake hayategemei bendi hiyo ambayo ipo kwa ajili ya kukuza na kuendeleza vipaji sambamba na kuwasaidia kimaisha wasanii.

"Mimi ni mfanyabiashara bwana, sitegemei bendi hii tu nina mambo mengi ya kufanya, naweza hata kujikita katika kukiimarisha chama changu cha maopinduzi (CCM), siwezi kuyumbishwa na lolote", Alisema.

Aidha, Iron Lady huyo alisema pamoja na kuondoka huko bendi hiyo imebakiwa na wasanii 32 ambapo ndani yake kuna waimbaji, wacheza shoo na wapiga vyombo.

Comments