YUSUF MANJI ATETA NA WACHEZAJI YANGA


WAKATI hali katika klabu ya Yanga ikiwa bado si shwari mjumbe wa bodi ya udhamini na mfadhili wa klabu ya Yanga Yusuf Manji jana amekutana na wachezaji wa timu hiyo na kuwaweka sawa.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho, Manji amewataka wachezaji hao kutulia kwa kutofuatilia migogoro inayoendelea ambayo inaweza kuwaathiri katika utendaji wao wa kazi.
Manji aliwaambia wao wachezaji hawana budi kuelekeza akili zao katika mechi zao ili waweze kushinda na hatimaye kutwaa ubingwa, kinyume na hapo wanaweza kujikuta wanaharibikiwa.
Pamoja na hayo, Manji pia aliwataka wachezaji hao kutulia kuhusiana na deni lao la usajili dhidi ya uongozi kwani muda si mrefu mambo yatakuwa sawa.
“Pamoja na hali tete iliyopo ndani ya klabu yetu nawaomba mtulie na kufanya kinachotakiwa uwanjani, si mnajua mnakabniliwa na mechi za ligi na zile za kimataifa, sasa inabidi mtulie,” alisema.Kumekuwepo na msigano baina ya wanachama wa klabu hiyo kuhusiana na uwepo wa Manji ndani ya klabu hiyo.

Comments

  1. Nii kweli wachezaji walitakiwa wasihusishwe kabisa na mambo ya migogoro ya utawala, wao ndio mashine ya timu, wakivurunda, hakuna uzalishaji, kwahiyo watulie waweke mpira chini, matoke ya kiwa mazuri...ni kwa faida yao!

    ReplyDelete

Post a Comment