YANGA KUIBOMOA TP MAZEMBE

KATIKA kuhakikisha inafanya vema kwenye michuano ya kimataifa mwakani, klabu ya Yanga imepanga kuwabomoa vigogo wa soka barani Afrika timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imefahamika.

Habari kutoka Yanga zinasema wamepanga kusajili wachezaji kadhaa nyota wa timu hiyo ili kuimarisha kikosi chao mwakani kiweze kufanya vema katika michuano hiyo.

Chanzo hicho cha habari kiliiambia Sayari mapema wiki hii kwamba mpango huo unafanywa chini ya mfadhili wa timu hiyo Yusuf Manji ambaye amepania kuifanyia makubwa timu hiyo.

Kilieleza kuwa, pamoja na kuibomoa Mazembe, pia watasajili wachezaji wengine toka katika nchi tofauti ndani na nje ya bara la Afrika ambao wanaamini uwepo wao Yanga utailetea mafanikio.

Comments