WANA MWANZA ISAIDIENI TOTO AFRICAN

TOTO AFICAN YA MWANZA

WAKATI timu zinazoshiriki ligi kuu bara zikiwa katika maanzalizi ya hali ya juu za mzunguko wa pili wa ligi hiyo unaotarajiwa kuanza januari 22, klabu ya Toto African ya Mwanza ndo kwanza imeanza mazoezi jana, tena ya kuungaunga.

Hali hiyo inatokana na ukata iliyonayo timu hiyo ambapo uongozi umeshindwa kuwatumia fedha za nauli wachezaji wake waliopo nje ya jiji la Mwanza ili kwenda kuungana na wenzao katika mazoezi.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Choke Abeid amesema kuwa anawasiwasi na timu uyake kufanya vema katika mzunguko huo wa lala salama kwani utakluwa na ushindani mkubwa na hasa ikizingatiwa kuna timu zitatakiwa kushuka daraja.
"Wenetu wameshaanza mazoezi karibu mwezi na wengine zaidi, sisi ndio tumeanza jana tena tukiwa na wachezaji wachache, yaaani kufanya kwetu vema katika duru la pili itakuwa ni vigumu kwa kweli", Amesema Choke.

Comments