SIMBA, YANGA KURUDIANA MACHI 5

BAADHI YA WACHEZAJI WA SIMBA
BAADHI YA WACHEZAJI WA YANGA

VIGOGO vya soka nchini timu za Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana machi 5 mwaka huu katika mechi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu bara unaotarajiwa kuanza januari 15.

Timu hizo zitakutana katika dimba la Jamhuri mjini Morogoro ambapo Yanga ndio watakuwa wenyeji wa mchezo huo.

Katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo timu hizo zilikwaana katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na Simba wakiwa wenyeji ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Jerry Tegete.

Kwa mujibu wa ratiba ya mzunguko huo wa lala salama wa ligi hiyo ambayo imetolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, ratiba hiyo imezingatia maandalizi ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kwa ajili ya mechi ya mchujo ya kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Afrika Kati itakayopigwa nchini Machi 26 pamoja na tarehe za mechi za kirafiki za FIFA.

Comments