SIMBA VS YANGA HAPATOSHI ZENJI KESHO




VIGOGO vya soka nchini Simba na Yanga kesho vitakutana katika mecjhi ya fainali ya kombe la Mapinduzi itakayopigwa kwenye uwanja wa Aman Visiwani Zanzibar.


Mechi hiyo itakayopigwa usiku itakuwa na msisimko wa aina yake na hasa ikizingatiwa hiii itakuwa ni mara ya kwanza kwa watani hao wa jadi nchini kukutana tangu kuanza kwa mwaka mpya wa 2011.


Aidha, mechi hiyo itakuwa na upinzani mkubwa kutokana na historia ya timu hizo, huku pia Simba itataka kulip[iza kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mechi yao ya ligi kuu bara Oktoba 16 kwenye dimba la CCM Kirumba mwanza, huku Yanga nayo ikitaka kushinda ili kulinda heshima.


Yote kwa yote nani atacheka, nani atanuna itajulikana baada ya dakika 90 za mtanange huo.

Comments