PRECISION AIR YAMPIGA TAFU MISS PROGRESS INTERNATIONAL 2010



SHIRIKA la ndege la Precision Air leo limeingia mkataba wa kumsaidia Miss Progress International, Julieth William Lugembe ili aweze kufanya kazi zake.
Meneja Masoko wa Shirika hilo Emilian Rwejuna amesema kwamba wameamua kumpiuga tafu mrembo huyo ili aweze kutimiza ndoto zake za kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi.

Julieth ambaye alishinda taji hilo nchini Italy, mwaka jana aliandika mchanganuo wa kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi 'Albino' ambapo zinahitajika kiasi cha sh milioni 40 ili kufanikisha mambo mbalimbali juu ya watu hao.
Julieth anatarajia kuzunguka mikoa mbalimbali Tanzania kuanzia Januari 15 mwaka huu ili kutembelea vituo vyenye kuhudumia watu hao na baadae kutoa misaada mbalimbali.

Comments