NENDA PAPIC, YANGA ITAENDELEA KUWEPO

MWENYEKITI WA YANGA LLOYD NCHUNGA KUSHOTO AKIWA NA MSEMAJI WA TIMU HIYO LOUIS SENDEU
SIKU moja baada ya kocha mkuu wa Yanga Kostadin Papic 'Clinton' kumwaga manyanga kuifundisha timu hiyo, mwenyekiti wa timu hiyo Lloyd Nchunga mesema kwamba kujitoa kwake hakuwezi kuipunguzia lolote timu hiyo.

Nchunga alisema Yanga itaendelea kuwepo kwani yeye si wa kwanza wala wa mwisho kuifundisha klabu hiyo, hivyo wanayanga hawana budi kutuliza akili zao badala ya kumfikiria Papic.

Alisema Yanga kwa sasa itakuwa chini ya kocha msaidizi Fred Felix Minziro ikiendelwea na maandalizi ya mechi yake ya kombe la Shirikiso la Soka Barani Afrika (CAF) jumamosi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Papic alitanga kujiuzuru jana kutokana na kuopinga ujio wa Minziro kama msaidizi wake.

Comments