MSHINDI BSS 2010 ADAI MILIONI 30 ALIZOZAWADIWA NI VIJISENTI TU



MSHINDI wa shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search (BSS) kwa mwaka 2010, Mariam Mohammed, amesema kwamba kitita cha shilingi za kitanzania milioni 30 alichokipata kama zawadi ya ushindi huo kwake ni sawa na vijisenti.
Mariam aliyanena hayo usiku wa Desemba 29 nyumbani kwao Mabibo Mzambarauni wakati akisherehekea ushindi wake.
“Najua wengi hamkupenda nishinde lakini nimeshinda, kwanza kwangu milioni 30 si chochote na ndiyo sababu sikuzuzuka kwenda kuvichukua siku niliyohitajika kwenda kuchukua, kwani vijihela hivyo nimezoea kuvishika kila wakati”.Alisema

Comments