KOCHA WA STARS AWAPOZA WATANZANIA MICHUANO YA MTO NILE


Na MWANDISHI Maalum, Cairo
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen amewapoza Watanzania kwa kuwaambia kushindwa kwa timu hiyo kuingia nusu fainali ya michuano ya Nchi za Bonde la Mto Nile kusiwakatishe tamaa kwani timu ni nzuri ila ilikosa umakini kwa baadhi ya mechi.Alitoa kauli hiyo baada ya juzi Stars kufungana bao 1-1 na Uganda katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi katika michuano hiyo, hivyo kuishia kuwania mshindi wa tano kesho.Poulsen alisema jana mjini hapa kuwa mechi zote ilizocheza Stars, ni makosa madogo ndiyo yaliyoigharimu timu, hvyo kuna haja ya kulifanyia kazi jambo hilo.Hata hivyo alisema Stars ilicheza vizuri na kwamba si sahihi kusema ilicheza vibaya, ila ilishindwa kuzitumia nafasi chache ilizopata kufunga na pia ilikosa umakini katika kulinda lango lake."Nimesikitishwa sana kushindwa kufuzu nusu fainali, lakini ndiyo soka lilivyo na jirani zetu Uganda na Kenya wao wameingia huo ndiyo mchezo ulivyo," alisea kocha huyo raia wa Denmark.Alisema mechi ya juzi dhidi, Stars ilifanikiwa kuwamiliki vyema wapinzani wake, lakini tatizo la umakini hasa katika safu ya ulinzi na pia kushindwa kuzitumia nafasi za kufunga ilizopata lilikuwa kikwazoLakini aliwaomba Watanzania wasikatishwe tamaa na matokeo hayo, kwani bado anajenga kikosi imara kwa ajili ya michuano ya kuwania kufuzu fainali za Afrika mwakani.Naye nahodha wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa alieleza kufadhaishwa na matokeo hayo, lakini akisema ndivyo soka lilivyo kuna kushinda, kufungwa na sare.Stars juzi ilifungana bao 1-1 na Uganda katika mchezo wa mwisho hatua ya makund, matokeo ambayo yaliipeleka nusu fainali Uganda ikiwa na pointi nne nyuma ya Misri yenye pointi tisa ambayo juzi ilifunga Burundi mabao 3-0. Stars ni ya tatu ina pointi mbili na Burundi ni ya mwisho ina pointi moja iliyoipata kwa Stars.Stars katika michuano hii ilifungwa mabao 5-1 na Misri, ikafungana bao 1-1 na Burundi na matokeo kama hayo na Uganda.Kutokana na kushika nafasi ya tatu Kundi A, Stars kesho itacheza na Sudan ambayo ni ya tatu Kundi B kutafuta mshindi wa tano. Burundi inabaki kuwa ya saba na timu itakayofungwa kati ya Stars na Sudani itakuwa ya sita, ambazo pia zina zawadi zake.Nusu fainali inatarajiwa pia kufanyika kesho ambapo Misri itacheza na Kenya iliyoshika nafasi ya pili Kundi B, huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliyongoza Kundi B baada ya juzi kuifunga Sudani mabao 2-1 itaceza na Uganda.

Comments